Israel inaendelea kulipatia silaha jeshi la Myanmar
https://parstoday.ir/sw/news/world-i34893-israel_inaendelea_kulipatia_silaha_jeshi_la_myanmar
Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel unaendelea kusafirisha silaha kuelekea Myanmar kwa ajili ya jeshi la nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 27, 2017 04:17 UTC
  • Israel inaendelea kulipatia silaha jeshi la Myanmar

Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel unaendelea kusafirisha silaha kuelekea Myanmar kwa ajili ya jeshi la nchi hiyo.

Gazeti la Haretz linalochapishwa Israel limefichua habari hiyo kwa kuandika kuwa licha ya ripoti mbalimbali zilizotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kimbari yanayofanywa na jeshi la Myanmar dhidi ya jamii ya wachache ya Waislamu Warohingya, utawala wa Kizayuni wa Israel bado haujasitisha kusafirisha silaha kuelekea Myanmar.

Haretz limefafanua kuwa siku ya Jumatatu Mahakamu Kuu ya Israel ilikuwa na kikao cha kujadili ombi lililowasilishwa mbele ya mahakama hiyo la kutaka Israel isimamishe usafrishaji silaha kuelekea Myanmar, kikao ambacho kilihudhuriwa pia na mwakilishi wa serikali ya utawala haramu wa Kizayuni. Kwa mujibu wa gazeti hilo, mwakilishi huyo wa serikali alitamka kwamba haipasi vyombo vya mahakama kuingilia masuala ya nje.

Rais wa utawala wa Kizayuni Reuven Rivlin (kushoto) alipokutana na Jenerali  Min Aung Hlaing huko Tel Aviv 

Kitambo nyuma gazeti hilo la Israel liliripoti kuwa Jenerali  Min Aung Hlaing, mmoja wa makamanda wa jeshi la Myanmar alifanya safari huko Israel mwezi Septemba mwaka 2015 ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel Reuven Rivlin na wakuu wa mashirika ya uundaji silaha katika utawala huo. Katika safari yake hiyo, Jenerali HIaing alisaini mikataba kadhaa ya kununua silaha kutoka Israel.../