Oct 16, 2017 16:37 UTC
  • Marais wa nchi za Amerika ya Latini wakipongeza chama tawala Venezuela kwa kuwashinda wapinzani marafiki wa Magharibi

Marais wa nchi za Bolivia, Nicaragua na Cuba sambamba na kukaribisha ushindi wa chama tawala cha Kisosholisti nchini Venezuela kwa kuibuka mshindi katika uchanguzi wa magavana wa majimbo ya nchi hiyo uliofanyika Jumapili ya jana, wamefurahishwa pia na umoja na mshikamano wa Wavenezuela dhidi ya njama za Wamagharibi.

Rais Evo Morales wa Bolivia, Daniel Ortega wa Nicaragua na Raúl Castro wa Cuba kwa nyakati tofauti wametuma jumbe zao za pongezi kwa uongozi wa chama tawala nchini Venezuela (PSUV) kwa kushinda uchaguzi wa jana. Uchaguzi wa magavana wa majimbo ya Venezuela wa Jumapili ya jana, ulihudhuriwa na waangalizi 70 wa kimataifa ambao walifika katika vituo vya kupigia kura katika nchi yote.

Upigajikura ulivyokuwa.

Kwa mujibu wa ripoti, katika majimbo 23 ya Venezuela raia wengi wa nchi hiyo walijitokeza kwa wingi katika shughuli ya upigaji kura, licha ya kwamba awali wapinzani wanaoungwa mkono na Umoja wa Ulaya na Marekani walikuwa wamewataka wananchi kususia uchaguzi huo. Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi nchini humo (CNE) imetangaza kuwa chama tawala cha Kisosholisti nchini Venezuela kimepata kura nyingi katika majimbo 17. Aidha imetangaza kuwa uchaguzi huo umefanyika katika anga salama.

Wavenezuela wakishangilia ushindi wa serikali yao

Inafaa kuashiria kuwa, uchaguzi huo wa wakuu wa magavana wa majimbo ya nchi hiyo ulicheleweshwa kwa mwaka mzima kutokana na machafuko na maandamano ya wapinzani wanaoungwa mkono na Marekani na madola ya mengine ya Magharibi. Kwa mara kadhaa madola hayo ya Magharibi yamekuwa yakiendesha njama mbalimbali ikiwemo mashinikizo ya vikwazo, kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali ya nchi hiyo ambayo inapinga siasa za kupenda kujitanua za madola hayo.

Tags