Wanasiasa wa Ufaransa walaani kushiriki Macron katika mashambulizi dhidi ya Syia
Hatua ya Ufaransa ya kushiriki katika mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Uingereza dhidi ya Syria imekabiliwa na wimbi la malalamiko kutoka kwa wanasiasa wa nchi hiyo.
Marine Le Pen Mkuu wa chama cha mrengo wa kushoto cha Harakati ya Kitaifa ya Ufaransa ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa: Hatua ya Ufaransa kujiingiza katika vita vya Syria inaielekeza nchi hiyo katikia hali isiyotabirika.
Wakati huo huo Nicolas Bay mwanasiasa mwingine wa Ufaransa amesema kuwa hatua ya kijeshi dhidi ya serikali ya Syria ni jambo lisilokubalika na ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
Naye Jean-Luc Melanchon kutoka chama cha mrengo wa kushoto cha nchini Ufaransa ameeleza kuwa: Hatua ya Rais wa nchi hiyo ya kufuata siasa za Marekani haikubaliki na kwamba itazidisha mapigano.
Jean Pierre Lafaren Waziri Mkuu wa zamani wa Ufaransa wakati wa utawala wa Rais Jack Chirack amesema kuwa: Hakuna shaka kuwa matokeo ya mashambulizi ya kijeshi ya Marekani, Ufaransa na Uingereza huko Syria ni yatakuwa na uharibifu mkubwa zaidi.