Nikki Haley: Jeshi la Marekani haliondoki Syria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i43160-nikki_haley_jeshi_la_marekani_haliondoki_syria
Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa nchi hiyo haitaondoa wanajeshi wake huko Syria hadi itakapofikia malengo yake.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 16, 2018 04:33 UTC
  • Nikki Haley: Jeshi la Marekani haliondoki Syria

Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa nchi hiyo haitaondoa wanajeshi wake huko Syria hadi itakapofikia malengo yake.

Akizungumza na televisheni ya Fox News, Nikki Haley amesema kupatiwa dhamana ya kile amekitaja kuwa kutotumiwa silaha za kemikali ambazo ni hatari kwa maslahi ya Marekani, kuwa na uhakika wa kusambaratishwa Daesh na kupata vituo vinavyofaa kwa ajili ya kudhibiti harakati za Iran ni miongoni mwa malengo ya kuwepo Marekani huko Syria.  

Haley ameongeza kuwa Marekani haina lengo la kuwaondoa wanajeshi wake huko Syria hadi itakapokuwa na uhakika wa kufikiwa malengo yake hayo.

Wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Syria 

Hii ni katika hali ambayo Rais Donald Trump wa Marekani wiki iliyopita alitaka kuondoka wanajeshi wa Marekani huko Syria katika kipindi cha miezi sita ijayo na kabla ya kufanyika uchaguzi wa kongresi mwezi Novemba mwaka huu. Kabla ya hapo, Trump alisema kuwa wanajeshi wa Marekani karibuni hivi wataondoka Syria na kwamba Washington itaruhusu pande nyingine kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo ya Kiarabu.