Waziri Mkuu wa Uingereza apinga kunyongwa magaidi wa ISIS
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46968-waziri_mkuu_wa_uingereza_apinga_kunyongwa_magaidi_wa_isis
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema serikali yake itapinga vikali hukumu ya kuonyongwa magaidi wakufurishaji wa kundi la ISIS au Daesh ambao ni raia wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 23, 2018 09:35 UTC
  • Waziri Mkuu wa Uingereza apinga kunyongwa magaidi wa ISIS

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema serikali yake itapinga vikali hukumu ya kuonyongwa magaidi wakufurishaji wa kundi la ISIS au Daesh ambao ni raia wa nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi habari Jumatatu, msemaji wa waziri mkuu wa Uingereza amesema, "ni sera ya kimsingi ya serikali kupinga hukumu  ya kunyongwa."

Kauli hiyo imekuja baada ya ripoti za awali kuenea kuwa waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza alikuwa ameashiria kuwa serikali ya London itaafiki hukumu ya kunyongwa raia wawili wa nchi hiyo, Alezanda Kotey an El Shafee El Sheikh ambao ni wanachama wa kundi al kigaidi la ISIS wanaotuhumiwa kujiunga na kundi hilo nchini Syria.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

Msemaji wa May amepinga dhana hiyo na kusema wanatafakari adhabu kali lakini si ya kifo. Kotey na El Shafee wanatuhumiwa kuwa walihusika katika kuwachukua mateka raia wa nchi za Magharibi nchini Syria wakiwemo waandishi habari Wamarekani James Foley na Steven Soltoff.

Uingereza sawa na nchi za Ulaya hasa Ufaransa na Ujerumani zina idadi kubwa ya raia wao waliojiunga na makundi ya kigaidi hasa ISIS nchini Syria na Iraq.