FATF yakataa uanachama wa Saudia, Riyadh bado inafadhili ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48518-fatf_yakataa_uanachama_wa_saudia_riyadh_bado_inafadhili_ugaidi
Saudi Arabia imekataliwa uanachama kamili katika Shirikisho la Kupambana na Fedha Chafu na Ufadhili wa Makundi ya Kigaidi (FATF), ambayo ni bodi ya kimataifa ya kupambana na fedha chafu na ufadhili wa kifedha wa makundi ya kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 01, 2018 23:41 UTC
  • FATF yakataa uanachama wa Saudia, Riyadh bado inafadhili ugaidi

Saudi Arabia imekataliwa uanachama kamili katika Shirikisho la Kupambana na Fedha Chafu na Ufadhili wa Makundi ya Kigaidi (FATF), ambayo ni bodi ya kimataifa ya kupambana na fedha chafu na ufadhili wa kifedha wa makundi ya kigaidi.

Shirika la FATF limetangaza kuwa, Saudi Arabia umeshindwa kukamilisha viwango vinavyohitajika vya kupambana na utakatishaji wa fedha chafu na kufadhili makundi ya kigaidi. 

Uamuzo wa nchi zote 37 wanachama wa shirika hilo la kimataifa umetoa pigo kubwa kwa jitihada zinazofanywa na utawala wa kifalme wa Riyadh za kutaka kusafisha sura yake kama mfadhili na muungaji mkono mkubwa wa makundi ya kigaidi na ya Kiwahabi duniani.  

Utawala wa Saudi Arabia unafadhili makundi ya kigaidi.

Watawala wa Saudia walitarajia kwamba, mpango huo ungesaidia kuvutia wawekezaji wa kigeni na kukamilisha mpango wa kupanua uchumi wa nchi hiyo unaotegemea pato la mafuta ya petroli.

Saudia imenyimwa uanachama katika shirika la FATF baada ya tathmini kuthibisha kwamba, ilikuwa na kiwango cha chini cha ufanisi katika kupambana na utakatishaji wa fedha chafu na ufadhili wa makundi ya kigaidi.