Benki ya HSBC yajiunga na harakati ya kuisusia Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50486-benki_ya_hsbc_yajiunga_na_harakati_ya_kuisusia_israel
Benki mashuhuri ya HSBC ambayo ni ya saba kwa ukubwa duniani imesitisha ushirikiano wake na kampuni ya kuzalisha silaha ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya Elbit Systems, kutokana na ukiukaji wa haki za binadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 28, 2018 21:39 UTC
  • Benki ya HSBC yajiunga na harakati ya kuisusia Israel

Benki mashuhuri ya HSBC ambayo ni ya saba kwa ukubwa duniani imesitisha ushirikiano wake na kampuni ya kuzalisha silaha ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya Elbit Systems, kutokana na ukiukaji wa haki za binadamu.

Duru zilizo karibu na benki hiyo maarufu yenye makao makuu yake nchini Uingereza zimedokeza kuwa, benki hiyo imesitisha ushirikiano wake na kampuni hiyo ya kutengeneza ndege zisizo na rubani (drones) na mifumo ya silaha ya utawala haramu wa Israel.

Kundi la wanaharakati wa War on Want la Uingereza limesema benki ya HSBC imeamua kuisusia kampuni hiyo ya kuzalisha silaha ya Israel baada ya kupokea baruapepe  24,000 kutoka kwa watu walioonesha kutoridhishwa na ushirikiano wa benki hiyo na kampuni ya Elbit, inayozalisha silaha zinazotumiwa na jeshi la Israel kuwakandamiza wananchi wa Palestina.

Hata hivyo Benki ya HSBC haijatoa taarifa rasmi ya kutangaza uamuzi huo wa kuisusia kampuni hiyo ya kuzalisha silaha ya Israel.

Vuguvugu la kutaka kususiwa na kuwekewa vikwazo Israel, tawi la Afrika Kusini

Harakati ya mashirika 190 ya Palestina inayojulikana kama Boycott, Divestment and Sanctions (BDS), ilianza kushinikiza kususiwa bidhaa na huduma za Tel Aviv kimataifa mwaka 2005, hadi pale itakapotekeleza wajibu wake kwa msingi wa sheria za kimataifa.

Mkuu wa Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini amewahi kusema kuwa, haki ya uhuru wa kujieleza watu wanaotaka kushiriki katika kuisuia Israel inapaswa kuheshimiwa, na kwamba Ulaya inaunga mkono na kutetea uhuru wa kujieleza wa jumuiya na taasisi mbalimbali ikiwemo ile ya kuisuia Israel ya BDS.