Mwakilishi Mwislamu nchini Marekani apinga hoja yenye kuwaunga mkono Wazayuni
Mwakilishi Mwislamu wa Baraza la Wawakilishi nchini Marekani, amepinga hoja iliyowasilishwa na Seneta mmoja wa nchi hiyo ya kuwaunga mkono Wazayuni.
Rashida Tlaib, Mwakilishi Mwislamu mwenye asili ya Palestina na ambaye amechaguliwa hivi karibuni katika Baraza la Wawakilishi nchini Marekani amepinga hoja iliyowasilishwa na Marco Rubio, Seneta wa chama cha Republican, yenye lengo la kuunga mkono utawala huo katili. Tlaib ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter akihoji uaminifu na utetezi wa Warepblican kwa utawala huo khabithi, na kuandika kuwa Warepublican katika Baraza la Seneti la Marekani wamesahau kama wao ni wawakilishi wa nchi gani.
Katika hoja yake hiyo, Rubio ametaka kupigwa marufuku kushiriki mashirika ya Kimarekani katika harakati dhidi ya Israel inayoitwa 'Kususiwa, Kuzuiliwa na Kuwekewa Vikwazo Israel (BDS).' Harakati hiyo inatafuta uungaji mkono wa kimataifa kwa ajili ya kuhitimisha ukandamizaji wa Wazayuni dhidi ya Wapalestina kupitia njia ya kuziwekea vikwazo kimataifa bidhaa zinazozalishwa na Israel. Wanaharakati wa kiraia na wasomi wa vyuo vikuu nchini Marekani na Ulaya wameanzisha harakati pana kwa ajili ya kuzisusia bidhaa za Israel.