Magaidi wa MKO wanafundishwa jinsi ya kukata watu vichwa Albania
https://parstoday.ir/sw/news/world-i51610-magaidi_wa_mko_wanafundishwa_jinsi_ya_kukata_watu_vichwa_albania
Jarida la Ujerumani la Der Spiegel limefichua kuwa, wanachama wa genge la kigaidi la MKO lenye historia ya kufanya ugaidi, mauaji na jinai kubwa dhidi ya wananchi na viongozi wa Iran wanapewa mafunzo ya kutisha kama kuua watu kwa kuwakata vichwa nchini Albania.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 17, 2019 04:41 UTC
  • Magaidi wa MKO wanafundishwa jinsi ya kukata watu vichwa Albania

Jarida la Ujerumani la Der Spiegel limefichua kuwa, wanachama wa genge la kigaidi la MKO lenye historia ya kufanya ugaidi, mauaji na jinai kubwa dhidi ya wananchi na viongozi wa Iran wanapewa mafunzo ya kutisha kama kuua watu kwa kuwakata vichwa nchini Albania.

Kwa mujibu wa jarida hilo, wanachama wa genge hilo wanapokea mafunzo mbalimbali katika kambi iliyoko umbali wa kilomita 35 kutoka mji mkuu wa Albania, Tirana, ikiwemo jinsi ya kuua kwa kuchinja, kunyofoa jicho kwa kutumia vidole vya mkono, kuchana mdomo na kuvunja mkono.

Jarida hilo limewahoji wanachama walioliasi kundi hilo la MKO ambao wameliambia kuwa, baadhi ya wanachama waliowaacha kambini wanateswa vibaya na kusababishiwa matatizo za kisaikolojia.

Jarida la Ujerumani la Der Spiegel baada ya mahojiano na wanachama 15 walioko katika kambi hiyo nchini Albania limefichua kuwa, kambi hiyo ambayo ukubwa wake ni mara 50 ya uwanja wa soka ina wanachama wapatao 2000 wanaofunzwa mbinu hizo za ukatili.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Albania imekataa kuelieleza jarida la Der Spiegel sababu za kuliunga mkono genge hilo la kigaidi.  

Wanachama wa MKO kwenye mkutano

Mbali na nchi kadhaa za Ulaya, Shirika la Ujasusi la Utawala wa Kizayuni wa Israel MOSSAD limewahi kujitokeza hadharani na kukiri kuhusu ushirikiano wake na kundi la kigaidi la MKO, katika kupanga njama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mwaka jana pia, Massoud Khodabandeh, mwanachama mwandamizi wa genge hilo la kigaidi alifichua katika mahojiano na tovuti ya habari ya Jordan ya al Bawwaba kwamba, utawala wa Aal Saud unashirikiana na kundi hilo, na wakati fulani ulilipa tani tatu za dhahabu, masanduku matatu yaliyojaa saa za kifakhari aina ya Rolex na vito vingine vya thamani kubwa.