Mashtaka manane dhidi ya Trump kuwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani
Mjumbe mwandamizi wa kamati ya Intelijensia ya Baraza la Wawakilishi la Marekani amesema mashtaka manane ya tuhuma dhidi ya rais Donald Trump yatawasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo.
Devin Nunes, ambaye ni mjumbe wa chama cha Republican katika kamati hiyo amesema, tuhuma hizo nane zinazohusu mazungumzo ya simu aliyofanya Trump na marais na viongozi wa nchi kadhaa duniani zitafikishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani, William Barr.
Kwa mujibu wa mjumbe huyo mwandamizi wa kamati ya Intelijensia ya Baraza la Wawakilishi la Marekani, mafaili ya mashtaka hayo yanahusu mazungumzo ya simu aliyofanya Trump, yakiwemo yale aliyofanya na Rais Vladimir Putin wa Russia na Rais Enrique Peña Nieto wa Mexico.
Devin Nunes amebainisha kuwa: Mazungumzo ya simu aliyofanya Michael Flynn, mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Trump na balozi wa wakati huo wa Russia mjini Washington ni miongoni mwa mashtaka yatakayowasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani.
Nunes ameongeza kuwa: Kwa kuwa baadhi ya yale yaliyomo kwenye faili la mashtaka hayo ni masuala ya siri, hawezi kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu masuala hayo.
Mazungumzo ambayo Trump alifanya na Putin mwaka uliopita wa 2018 nayo pia yalikosolewa vikali na Wademocrat na baadhi ya Warepublican, ambao walisema, mwenendo ulioonyeshwa na rais wa Marekani katika mazungumzo hayo ulikwenda kinyume na itifaki za kiusalama.../