Waislamu wa Ufaransa ni wahanga wa ubaguzi wa kidini
(last modified Thu, 07 Nov 2019 12:43:06 GMT )
Nov 07, 2019 12:43 UTC
  • Waislamu wa Ufaransa ni wahanga wa ubaguzi wa kidini

Karibu nusu ya Waislamu wanaoishi nchini Ufaransa, ni wahanga wa vitendo vya ubaguzi.

Radio France Info imeripoti habari ya ongezeko la vitendo vya ubaguzi dhidi ya Waislamu wanaoishi nchi hiyo ya Magharibi kupitia ukurasa wake wa Twitter na kuandika kuwa, kila Waislamu 10 nchini Ufaransa, zaidi ya watu wanne kati yao wameripoti kuwa wahanga wa vitendo vya ubaguzi wa kidini dhidi yao. Siku chache zilizopita pia, Jean-Luc Antoine Pierre Mélenchon, mwenyekiti wa chama cha La France Insoumise (Ufaransa Haisalimu Amri) alimtuhumu Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo kwa kuchochea chuki dhidi ya Waislamu.

Jamii ya Waislamu nchini Ufaransa inabaguliwa

Mwanasiasa huyo, amesema kuwa tabia ya kuwatupia lawama Waislamu wa Ufaransa, inapasa kukomeshwa. Ufaransa ni nchi yenye jamii kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya, ambapo licha ya serikali ya Paris kujiepusha kutangaza takwimu rasmi za jamii ya Waislamu, nchi hiyo inakadiriwa kuwa na Waislamu milioni sita.