Onyo kuhusu hatari ya kuenea ugaidi wa ndani nchini Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i58207-onyo_kuhusu_hatari_ya_kuenea_ugaidi_wa_ndani_nchini_marekani
Hata kama kufuatia mashambulio ya Septemba 11 nchini Marekani nchi hiyo ilijinadi kuwa kinara wa mapambano dhidi ya ugaidi duniani na kutekeleza mashambulizi kadhaa ya kibabe katika pembe tofauti za dunia kufuatia madai hayo ya uongo, lakini kuenea kwa vitendo vya utumiaji silaha nchini humo, kumewapelekea watawala wa nchi hiyo kutoa tahadhari kuhusiana na kuenea ugaidi katika nchi hiyo ya Magharibi.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Dec 30, 2019 23:14 UTC
  • Ugaidi wa ndani nchini Marekani
    Ugaidi wa ndani nchini Marekani

Hata kama kufuatia mashambulio ya Septemba 11 nchini Marekani nchi hiyo ilijinadi kuwa kinara wa mapambano dhidi ya ugaidi duniani na kutekeleza mashambulizi kadhaa ya kibabe katika pembe tofauti za dunia kufuatia madai hayo ya uongo, lakini kuenea kwa vitendo vya utumiaji silaha nchini humo, kumewapelekea watawala wa nchi hiyo kutoa tahadhari kuhusiana na kuenea ugaidi katika nchi hiyo ya Magharibi.

Kuhusiana na suala hilo na baada ya kujiri shambulio lililotekelezwa siku ya Jumamosi usiku katika nyumba ya kuhani mmoja wa Kiyahudi nje ya mji wa New York, ambapo watu wasiopungua watano walijeruhiwa, maafisa wa ngazi za juu wa Marekani wametahadharisha kuhusiana na hatari ya kuenea ugaidi wa ndani nchini humo. Akizungumza Jumapili mara tu baada ya kutokea shambulizi hilo la silaha baridi, Andrew Cuomo, Gavana wa New York alisema mbele ya makuhani wa eneo hilo kwamba tukio hilo lilikuwa la kigaidi. Alisema washabmbuliaji ni Wamarekani ambao walikuwa na nia ya kuibua woga na hofu nchini humo. Nukta ya kuzingatiwa hapa ni kuwa katika radiamali yake kuhusiana na suala hilo, Rais Donald Trump wa Marekani hakuashiria hata kidogo ugaidi wa jambo hilo bali alisema kuwa tukio hilo lililotokana na chiki dhidi ya Mayahudi. Hii ni katika hali ambayo katika miaka ya karibuni mashambulio mabaya zaidi kuliko hilo yamekuwa yakifanyika na kuongezeka dhidi ya Waislamu na wala hajawahi kusema kuwa yametokana na chuki dhidi ya Waislamu.

Andrew Cuomo, Gavana wa jimbo la New York

Msusuru wa matukio ya mauaji ya kutisha ambayo yamekuwa yakiorodheshwa na polisi ya upelelezi ya Marekani FBI yametajwa kuwa ya kigaidi jambo ambalo limepelekea kutolewa maonyo ya kuongezeka vitendo vya ugaidi wa ndani katika nchi hiyo. Mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu, wakurugenzi sita wa zamani wa ngazi za juu katika mapambano dhidi ya ugaidi katika Baraza la Usalama wa Taiafa la Marekani walitoa taarifa wakiwataka viongozi wa nchi hiyo kuchukua hatua za dharura kwa ajili ya kupambana na tatizo hilo. Waliitaka serikali kuu ya Marekani kutenga bajeti maalumu kwa lengo la kuzuia fikra za kupindukia mipaka na kila aina ya matumizi ya mabavu yanayotokana na kila itikadi inayolenga jamii ya Marekani.

Chanzo cha ugaidi wa ndani nchini Marekani kinarejea nyuma makumi ya miaka ambapo makundi na raia kadhaa wa nchi hiyo wamehusika na vitendo vya kutisha vya ugaidi. Moja ya matukio hayo ni kulipuliwa jengo la federali la Alfred P. Murrah katika mji wa Oklahoma mnamo mwaka 1995. Mlipuko huo ulitekelezwa na kundi moja la wanamgambo wa Marekani ambao walikuwa wakilalamikia siasa za serikali kuu. Ama kwa kweli, baadhi ya matukio muhimu ya ugaidi wa ndani nchini Marekani yametekelezwa na watu na makundi ya wanamgambo walio na fikra za kihafidhina na za mirengo ya kulia. Makundi hayo ni pamoja na ya watu wanaounga mkono serikali za majimbo kupewa madaraka zaidi na kupinga serikali kuu, makundi ya ubaguzi wa rangi yanayopinga jamii za wachache na dini zao na makundi ya wapinzani dhidi ya wahamiaji ambayo yanataka watu weupe wapewe fursa na haki zaidi kuliko jamii na raia wengine wa Marekani. Suala hilo lilidhihiri wazi katika mauaji ya umati yaliyotekelezwa na Patrick Crusius tarehe 3 Agosti mwaka huu dhidi ya wahahiri wa Amerika ya Latin katika mji wa El Paso jimboni Texas, ambapo alitangaza wazi kwamba alikuwa mfuasi wa siasa za Rais Donald Trump zinazopinga wahajiri kuingia nchini humo.

Mauaji ya umati yaliyotekelezwa eneo la El Pasom Texas nchini Marekani

Ripoti na takwimu zinaonyesha kwamba vitendo vya mashambulio na mauaji dhidi ya jamii za waliowachache kirangi na kidini vimeongezeka Marekani katika miaka ya hivi karibuni, yaani tokea aingie madarakani Donald Trump. Ni wazi kuwa vyombo vya habari vya nchi hiyo pia vimechochea pakubwa ugaidi na ubaguzi dhidi ya jamii hizo za waliowachache. Kwa mujibu wa Pete Buttigieg, mwanasiasa mashuhuri wa Marekani, nchi hiyo inashuhudia ongezeko la mashambulio ya kigaidi na ya ubaguzi wa rangi yanayotekelezwa na weupe wabaguzi wa rangi wenye fikra za utaifa ambao wanachochewa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo.

Rais huyo wa Marekani aliye na chuki kubwa dhidi ya wageni amekuwa akitoa matamshi ya kichochezi dhidi ya wahamiaji wasio na nyaraka na pia jamii za waliowachache kirangi na kidini na hasa wanaotoka Amerika ya Latini na nchi za Kiislamu.