Ujerumani yaitaka Saudi Arabia ichunge haki za binadamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i59311-ujerumani_yaitaka_saudi_arabia_ichunge_haki_za_binadamu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amewataka viongozi wa Saudi Arabia wafanyie marekebisho sheria zao na wachunge haki za binadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 22, 2020 03:50 UTC
  • Ujerumani yaitaka Saudi Arabia ichunge haki za binadamu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amewataka viongozi wa Saudi Arabia wafanyie marekebisho sheria zao na wachunge haki za binadamu.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Heiko Maas, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, jana Ijumaa alionana na waziri mwenzake wa Saudia, Faisal bin Farhan Aal Saud mjini Berlin, Ujerumani na kumwambia kwamba njia pekee ya kulindwa haki za binadamu ni kushirikishwa wananchi katika maamuzi ya nchi huko Saudia, suala ambalo linaweza kuleta mabadiliko mazuri nchini humo.

Maas amegusia pia mazungumzo ya pande mbili za Ujerumani na Saudi Arabia kuhusu matukio ya eneo hili yakiwemo ya Iraq, Syria na Yemen na kusema kuwa, Riyadh ina nafasi kubwa sana katika masuala hayo. Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema kuwa, mazungumzo yake na waziri mwenzake wa Saudi Arabia yamehusu pia Iran.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumaini na Saudi Arabia

 

Saudia imeanzisha mashambulizi ya pande zote dhidi ya wananchi maskini wa Yemen na imewafanyia jinai kubwa wananchi hao Waislamu. Mara kwa mara Saudi Arabia imekuwa ikishutumiwa kwa kufanya ukatili mkubwa katika nchi mbalimbali kama vile Yemen na Syria.

Hadi hivi sasa uvamizi wa Saudi Arabia nchini Yemen umeshaua watu wasiopungua 16 elfu huku ripoti za Umoja wa Mataifa zikionesha kuwa, ukame uliosababishwa na uvamizi huo huko Yemen ni janga kubwa zaidi la kibinadamu duniani.