Baraza la Mamufti Russia lamshukuru Kiongozi Muadhamu kwa kuwatetea Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i59479-baraza_la_mamufti_russia_lamshukuru_kiongozi_muadhamu_kwa_kuwatetea_wapalestina
Baraza la Mamufti la Russia limempongeza na kumshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei kwa kutetea haki halali za Wapalestina.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 01, 2020 08:09 UTC
  • Baraza la Mamufti Russia lamshukuru Kiongozi Muadhamu kwa kuwatetea Wapalestina

Baraza la Mamufti la Russia limempongeza na kumshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei kwa kutetea haki halali za Wapalestina.

Katika mkutano na Kazem Jalali, Balozi wa Iran mjini Moscow, Mkuu wa Baraza la Mamufti la Russia Ravil Gainutdin amesema baraza hilo linajivunia kuwa na uhusiano mzuri na Iran na kusisitiza kuwa ushirikiano huo umekuwa na taathira chanya katika masuala muhimu ya kieneo.

Ravil Gainutdin amesema, "uhusiano mzuri baina ya Iran na Russia katika nyuga za siasa, uchumi na utamaduni unapaswa kuimarishwa. Waislamu wa Russia wanaunga mkono uhusiano huo ambao umezaa matunda katika kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria."

Mkuu wa Baraza la Mamufti la Russia ameeleza bayana kuwa, Marekani na nchi za Ulaya zinatiwa kiwewe na uhusiano wa Tehran na Moscow, na ndiposa zimeziwekea vikwazo Iran, Russia, Uturuki na China kwa kuwa wanafahamu kuwa uhusiano huo ni tishio kwa uistikbari wa dunia.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Hivi karibuni, Baraza la Mamufti la Russia lilisema kuwa Waislamu wanapasa kuwaunga mkono Wapalestina dhidi ya mpango wa Kimarekani wa Muamala wa Karne.

Baraza hilo limesema nchi zote za Kiarabu na Kiislamu zinapasa kuwaunga mkono Wapalestina na kuhitimisha ukiukaji wa haki za taifa hilo.