Putin: Moscow haina nia ya kuingia vitani na nchi yoyote
https://parstoday.ir/sw/news/world-i59506-putin_moscow_haina_nia_ya_kuingia_vitani_na_nchi_yoyote
Rais Vladimir Putin wa Russia ametoa radiamali yake kufuatia kushtadi mizozo kati ya nchi yake na Uturuki kuhusiana na kadhia ya Idlib, Syria na kusisitiza kwamba, Moscow haina nia ya kuingia vitani na nchi yoyote.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 02, 2020 10:07 UTC
  • Vladimir Putin
    Vladimir Putin

Rais Vladimir Putin wa Russia ametoa radiamali yake kufuatia kushtadi mizozo kati ya nchi yake na Uturuki kuhusiana na kadhia ya Idlib, Syria na kusisitiza kwamba, Moscow haina nia ya kuingia vitani na nchi yoyote.

Rais Putin ameyasema hayo katika mahojiano na shirika la habari la TASS na kuongeza kwamba, Moscow inata kuwepo mazingira ambayo hayataruhusu kuwepo vita kati nchi yoyote na Russia. Matamshi hayo ya Rais wa Russia yametolewa baada ya kuongezeka mzozo kati ya Moscow na Ankara kuhusiana na suala la Idlib, Syria. Kuendelea kusonga mbele jeshi la Syria kwa lengo la kuzikomboa ngome kuu za magaidi katika mikoa ya Idlib na Aleppo, kaskazini magharibi mwa Syria, kumezidisha mgogoro wa kijeshi kati ya Uturuki na Syria.

Uturuki, muungaji mkono mkubwa wa makundi ya kigaidi nchini Syria

Serikali ya Uturuki sambamba na kupinga operesheni hiyo, imefikia hata hatua ya kuvamia sehemu ya ardhi ya Syria na kuendelea kuyaungaji mkono makundi ya kigaidi. Hatua hiyo imekabiliwa na radiamali kali ya Russia ambayo, kwa mwaliko rasmi wa Damascus, inaisaidia serikali ya Rais Bashar al-Assad katika operesheni zake dhidi ya makundi ya kigaidi.