Macron akiri kuwepo uhaba wa suhula za kitiba nchini Ufaransa
Rais wa Ufaransa amesema kuwa nchi hiyo inakabiliwa na tatizo la kudhamini vifaa vya tiva vya dharura kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya corona.
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema baada ya kutembelea kiwanda kimoja cha kutengeneza barakoa(mask) kwamba nchi hiyo inakabaliwa na uhaba wa barakoa na vifaa vya kusaidia wagonjwa kupumua na pia katika kudhamini baadhi ya dawa za matibabu.
Rais wa Ufaransa aidha amesisitiza kuhusu kutengeneza jumla ya barakoa milioni 15 kwa wiki. Rais Emmanuel Macron nwa Ufaransa Jumamosi iliyopita alitangaza kuwa hali ya karantini iliyowekwa nchini humo kutokana na maambukizo ya corona itarefushwa kwa wiki mbili zingine hadi tarehe 15 mwezi Aprili.
Mkuu wa muungano wa hospitali za Ufaransa awali alikuwa ametahadharisha kuhusu uhaba wa suhula na kuweko ulazima wa kushirikiana pande mbalimbali ili kukabiliana na maambukizo ya virusi vya corona nchini humo. Alitahadharisha kuwa iwapo hospitali au maeneo ya miji yatafanya kazi peke yake bila ya kushirikiana na sekta nyingine nchi hiyo itakabiliwa na janga kubwa.
Jumla ya watu 44,000 na 750 wameambukizwa virusi vya corona nchini Ufaransa hadi hivi sasa na wengine elfu tatu na 24 wameaga dunia kwa ugonjwa wa covid-19.