UN yataka kufanyika uchunguzi wa mauaji ya wahajiri 30 Libya
Umoja wa Mataifa umetoa mwito wa kufanyika uchunguzi wa mauaji ya makumi ya wahajiri huko nchini Libya.
Yacoub El Hillo, mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA) nchini Libya alitoa mwito huo jana Ijumaa, ambapo pia amelaani kuuawa kwa kupigwa risasi makumi ya wahajiri katika kituo kimoja cha biashara ya utumwa mambo le0.
Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya imetoa waranti ya kukamatwa washukiwa wa mauaji hayo karibu na mji mkuu Tripoli. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Libya, Fathi Bashagha amesema vyombo vya usalama vimeanzisha msako mkali wa kuwasaka wahusika wa mauaji hayo ya kutisha ya Jumatano iliyopita katika mji wa jangwani wa Mizda, yapata kilomita 160 kusini mwa Tripoli.
Jana Ijumaa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Bangladesh ilisema wahajiri 30 waliouawa katika tukio hilo walishikwa mateka na kuteswa vibaya kabla ya kuuawa. Wizara hiyo imemnukuu mmoja wa manusuru ambaye anasema miongoni mwa wahajiri waliouawa ni raia 24 wa Bangladesh na sita wa Kiafrika.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Bangladesh imeongeza kuwa, wahajiri hao walifanyiwa ukatili na mateso ya kila aina huku wakiitishwa pesa za kikomboleo.
Habari zaidi zinasema kuwa, wahajiri wengine 11 walionusurika ukatili huo wa Jumatano wamelazwa katika hospitali moja mjini Mizda. Ifahamike kuwa, mji wa Midza upo chini ya udhibiti wa vikosi vya jenerali muasi, Khalifa Haftar ambaye anaongoza kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya.