May 22, 2021 06:38 UTC
  • Hania: Mashahidi wa Palestina wamethibitisha kuwa Quds ni mstari mwekundu

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amegusia jinsi Wapalestina walivyouliwa shahidi na Wazayuni katika vita vya Quds na kusisitiza kuwa, mashahidi hao wamewathibitisha watu wote kwamba Quds na Msikiti wa al Aqsa ni mstari mwekundu kwa taifa hilo na umma wote wa Kiislamu.

Televisheni ya al Mayadeen imeripoti habari hiyo na kumnukuu Ismail Hania akisisitiza kuwa, muqawama wa kishujaa wa Wapalestina ni ushindi mkubwa wa kiistratijia kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Amesema, tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliyelifungulia taifa letu upeo na uwanda mpana wa kuingia katika awamu mpya ya historia ya umma huu.

Wakati huo huo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Palestina huko Ghaza imetangaza kuwa, utawala vamizi wa Kizayuni umeshambulia kinyama na kiwendawazimu viwanda, mashamba ya kilimo na taasisi za serikali ili kulishinikiza taifa la Palestina lisalimu amri, lakini utawala huo dhalimu umeshindwa kufikia malengo yake haramu.

Wapalestina, wakubwa kwa wadogo wanamwaga damu zao kwa ajili ya malengo matakatifu

 

Nayo talevisheni ya al Iraqiyyah imewanukuu maafisa wa Palestina wakisema kuwa, katika vita vya hivi sasa vya Saifil Quds, utawala wa Kizayuni umevunja kikamilifu nyumba 447 za Wapalestina kwenye Ukanda wa Ghaza.

Katika mashambulio yake hayo ya kihayawani, utawala wa Kizayuni umeharibu nyumba 13,000 za Wapalestina.

Maafisa wa Ukanda wa Ghaza vile vile wamesema, utawala wa Kizayuni wa Israel umeharibu kwa makusudi taasisi na miundombinu ya kutoa huduma kwa raia na taasisi za kiuchumi kama vile mfumo wa usambazaji maji safi ya kunywa na bara bara za Ukanda wa Ghaza.

Tags