Walinda amani wawili wa UN wauawa Mali
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1096-walinda_amani_wawili_wa_un_wauawa_mali
Askari wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wameuawa katika hujuma ya kigaidi kaskazini mwa Mali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 12, 2016 11:50 UTC
  • Walinda amani wawili wa UN wauawa Mali

Askari wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wameuawa katika hujuma ya kigaidi kaskazini mwa Mali.

Taarifa zinasema kuwa leo Ijumaa magaidi walihujumu kituo cha vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA, na kuwaua maafisa wawili wa kulinda amani na kuwajeruhi wengine 30.

Duru zinadokeza kuwa maafisa wawili waliouawa katika tukio la leo ni raia wa Guinea. Aidha imeelezwa kuwa askari saba waliojeruhiwa wako katika hali mahututi.

Hujuma ya leo inajiri wiki moja tu baada ya kushambuliwa kituo cha askari wa Nigeria katika kikosi cha Minusma katika hoteli moja ya kale mjini Timbuktu kaskazini mwa Mali. Kundi la kigaidi la al Qaeda lilitangaza kuhusika na hujuma huyo. Katika tukio hilo askari mmoja wa Mali aliuawa na washambuliaji wanne wakaangamizwa. Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa waliwasili Mali Juni mwaka 2013.