Wanawake Zimbabwe waandamana kumpinga Rais Mugabe
(last modified Sun, 17 Jul 2016 07:45:28 GMT )
Jul 17, 2016 07:45 UTC
  • Wanawake Zimbabwe waandamana kumpinga Rais Mugabe

Mamia ya wanawake nchini Zimbabwe jana walifanya maandamano dhidi ya serikali ya Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo kwa kupiga masufuria; kitendo kinashoashiria namna nchi hiyo inavyokabiliwa na njaa na matatizo ya kiuchumi.

Maandamano hayo yaliyoitishwa na Chama Kikuu cha Upinzani cha Harakati ya Mabadiliko ya Kidemokrasia (MDC), chini ya anwani ya "Kampeni ya Kupiga Masufuria", yamefanyika Bulawayo mji wa pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe.

Makamu Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha MDC, Thokozani Khupe amesema katika maandamano hayo kuwa masufuria hayo yanayopigwa na waandamanaji hayana kitu cha kupika majumbani ndio maana wameamua kuyabeba ili kueleza kuwa hawana chochote cha kupika na wanakabiliwa na njaa.

Wanawake hao ambao walikuwa wamevaa sare za rangi nyekundu ya chama cha MDC walibeba mabango yanayomshutumu Rais Mugabe na kumtaka aondoke madarakani. Maandamano hayo ya mamia ya wanawake katika mji wa Bulawayo yametanguliwa na maandamano kadhaa kote nchini humo ya kulalamikia hali mbaya ya uchumi nchini Zimbabwe.

 

 

Tags