Matamshi ya afisa jeshi wa Libya kuhusu kuweko nchini vikosi ajinabi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i11806-matamshi_ya_afisa_jeshi_wa_libya_kuhusu_kuweko_nchini_vikosi_ajinabi
Kamanda wa kikosi cha anga cha jeshi la Libya amesema kuwa wanajeshi wa Marekani, Uingereza na Ufaransa wapo Libya kwa ajili tu ya kudhibiti harakati za kundi la kigaidi la Daesh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 23, 2016 02:32 UTC
  • Matamshi ya afisa jeshi wa Libya kuhusu kuweko nchini vikosi ajinabi

Kamanda wa kikosi cha anga cha jeshi la Libya amesema kuwa wanajeshi wa Marekani, Uingereza na Ufaransa wapo Libya kwa ajili tu ya kudhibiti harakati za kundi la kigaidi la Daesh.

Saqr al Joroush Kamanda wa kikosi cha anga cha jeshi la Libya ameashiria kuwepo baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa, Marekani na Uingereza katika kituo cha anga cha Benina katika mji wa Benghazi na kueleza kuwa idadi ya wanajeshi hao inakaribia 20 na kwamba kazi yao ni kudhibiti harakati za kundi la kigaidi la Daesh. Kamanda wa kikosi cha anga cha jeshi la Libya ametangaza habari ya kuwepo makundi ya kijeshi ya nchi ajinabi katika kambi na miji mbalimbali huko Libya kama vile Tobrok, Misrata na Tripoli. 

 

Wanajeshi wa Ufaransa Libya 

Rais Francois Hollande wa Ufaransa siku tatu zilizopita aliripoti habari ya kuuliwa wanajeshi watatu wa nchi hiyo mashariki mwa Libya.  Hii ni mara ya kwanza ambapo Paris imekiri kuwepo wanajeshi wake huko Libya. 

Katika upande mwingine Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) mwezi Mei mwaka huu ilitangaza kuwa jeshi la nchi hiyo halina taswira ya wazi kuhusu hali ya mambo huko Libya, na hii ni katika hali ambayo timu ndogo za wanajeshi wa oparesheni maalumu wa Marekani hivi sasa wako Libya wakikusanya taarifa muhimu.