Sheikh Jalala awaasa Watanzania kuhurumiana na kupendana bila kujadli itikadi za kidini
(last modified Mon, 12 Dec 2016 02:39:31 GMT )
Dec 12, 2016 02:39 UTC
  • Sheikh Jalala awaasa Watanzania kuhurumiana na kupendana bila kujadli itikadi za kidini

Kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia Ithnashariya nchini Tanzania Shekh Hemed Jalala amewataka Watanzania kuwa na tabia ya kuhurumiana, hasa wenye uwezo kuwahurumia wasio na uwezo.

Sheikh Jalala aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa maelezo, ikiwa imesalia siku moja kufikia maadhimisho ya wiki ya umoja kwa Waislamu ambapo Waislamu wa Shia na Suni huadhimisha kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W). 

Sheikh Hemed Jalala akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam 

Akizungumza katika mkutano huo, Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa Mtume Muhammad (S.A.W) alifundisha kuwa dini imekuja kutunza upendo na amani; hivyo ni vyema Watanzania waishi kwa upendo bila kujali tofauti za dini zao. Ameongeza kuwa ni vyema jamii kuishi maisha aliyoishi Mtume Mtukufu ikiwa ni pamoja na sifa kuu mbili alizokuwa nazo yaani kuwa mkweli na mwaminifu.