Watu 26 waaga dunia baada ya mabasi 2 kugongana Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i28772-watu_26_waaga_dunia_baada_ya_mabasi_2_kugongana_nigeria
Kwa akali watu 26 wamepoteza maisha katika ajali mbaya ya barabarani katika mji wa Lagos magharibi mwa Nigeria.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 07, 2017 13:17 UTC
  • Watu 26 waaga dunia baada ya mabasi 2 kugongana Nigeria

Kwa akali watu 26 wamepoteza maisha katika ajali mbaya ya barabarani katika mji wa Lagos magharibi mwa Nigeria.

Adekunle Ajisebutu, msemaji wa polisi katika jimbo la Oyo amesema ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi baada ya mabasi mawili kugongana katika barabara kuu ya Lagos-Ibadan.

Ameongeza kuwa, abiria wengine 11 wamepata majeraha mabaya katika ajali hiyo na kwamba vyombo vya dola vinachunguza kiini cha ajali hiyo.  

Ajali iliyotokea mwaka jana 2017 Nigeria

Disemba mwaka jana, watoto 11 walipoteza maisha baada ya kugongwa na basi walipokuwa wakishiriki zefe (matembezi) ya Maulid  ya kukumbuka mazazi ya Mtume (SAW)  katika jimbo la Gombe, kaskazini mwa Nigeria. Zaidi ya watu elfu 5 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani nchini Nigeria mwaka jana pekee.

Nchi ya Nigeria imekuwa ikikumbwa na visa vya ajali za barabarani kutokana na hali mbaya za magari, barabara pamoja na kutozingatiwa sheria za barabarani.