Libya yataka kuondolewa vikwazo vya silaha
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i29520-libya_yataka_kuondolewa_vikwazo_vya_silaha
Waziri Mkuu wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya ametaka nchi yake iondolewe vikwazo vya silaha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 24, 2017 09:55 UTC
  • Libya yataka kuondolewa vikwazo vya silaha

Waziri Mkuu wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya ametaka nchi yake iondolewe vikwazo vya silaha.

Mtandao wa habari wa al Yaum al Sabi' wa nchini Misri imemnukuu Faiz al Sarraj, Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya akiwaambia waandishi wa habari mjini Tripoli kwamba, kuna udharura wa kuondolewa vikwazo vya silaha ilivyowekewa nchi yake ili vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo kama jeshi na polisi viweze kulinda usalama wa nchi hiyo. 

Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amesema, jeshi na polisi ya Libya inahitajia kujengwa upya, kupewa silaha, mafunzo ya kijeshi na kubadilishana taarifa za kijasusi.

Silaha zimeenea mikononi mwa makundi yenye silaha kila moja linagombania kudhibiti maeneo zaidi

 

Faez al Sarraj ameongeza kuwa, wananchi wa Libya hivi sasa wanateseka kwa matatizo mengi kwani nchi yao tangu miaka kadhaa nyuma imekumbwa na migogoro ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama.

Mwezi Februari 2011, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga marufuku Libya kuuziwa silaha za aina yoyote ile kutokana na kuongezeka machafuko ndani ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.