Magaidi 19 wa al Shabab wauawa Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i3223-magaidi_19_wa_al_shabab_wauawa_somalia
Jeshi la Kenya limetangaza kuwa wapiganaji 19 wa kund la kigaidi la al Shabab wameuawa huko kusini mwa Somalia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 17, 2016 03:48 UTC
  • Magaidi 19 wa al Shabab wauawa Somalia

Jeshi la Kenya limetangaza kuwa wapiganaji 19 wa kund la kigaidi la al Shabab wameuawa huko kusini mwa Somalia.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi la Kenya imesema kuwa, magaidi hao wa al Shabab walikuwa na nia ya kushambulia kambi ya askari wa wa Umoja wa Afrika AMISOM lakini walikumbana na askari wa Kenya wa kikosi hicho na 19 miongoni mwao wameuawa. Taarifa hiyo imesema idadi kadhaa ya silaha za magaidi hao pia zimechukuliwa ngawira.

Miezi iliopita kundi la kigaidi la al Shabab lilishambulia mara tatu kambi ya askari wa Umoja wa Afrika huko kusini mwa Somalia na kuua idadi isiyojulikana na askari wa Kenya.

Askari wa kulinda amani wa nchi za Kiafrika walitumwa Somalia mwaka 2007 kukabiliana na kundi la kigaidi la al Shabab na kurejesha amani na utilivu nchini humo.