Wanigeria waandamana, wamtaka Buhari ajiuzulu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i33122-wanigeria_waandamana_wamtaka_buhari_ajiuzulu
Wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano makubwa wakitaka Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo aliyeko London nchini Uingereza arejee nyumbani na kujiuzulu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 14, 2017 02:50 UTC
  • Wanigeria waandamana, wamtaka Buhari ajiuzulu

Wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano makubwa wakitaka Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo aliyeko London nchini Uingereza arejee nyumbani na kujiuzulu.

Wanigeria walifanya maandamano hao yaliyoitishwa na jumuiya za kiraia wakipinga kitendo cha rais wa nchi hiyo kuendelea kuishi nje ya nchi kwa kipindi cha miezi mitatu. Buhari anayesumbuliwa na maradhi ambayo hayajatangazwa rasmi, amelazwa katika hosptali moja mjini London.

Wakati huo huo Wizara ya Habari ya Nigeria imedai kuwa, hali ya kiongozi wa nchi hiyo ni nzuri. 

Wanigeria wakimtaka Buhari ajiuzulu

Tangu alipoondoka nchini Nigeria miezi mitatu iliyopita na kwenda Uingereza kwa matibabu, Rais Muhammadu Buhari hajawahi kufanya mahojiano na vyombo vya habari au kuonekana hadharani.