Watu 30 waaga dunia katika ajali mbaya ya barabarani nchini Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i34387-watu_30_waaga_dunia_katika_ajali_mbaya_ya_barabarani_nchini_nigeria
Kwa akali watu 30 wamepoteza maisha kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia leo kusini magharibi mwa Nigeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 15, 2017 09:32 UTC
  • Watu 30 waaga dunia katika ajali mbaya ya barabarani nchini Nigeria

Kwa akali watu 30 wamepoteza maisha kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia leo kusini magharibi mwa Nigeria.

Msemaji wa Mamlaka ya Usalama Barabarani nchini humo, Bisi Kazeem  amesema ajali hiyo ilitokea baada ya mabasi mawili ya abiria kugongana ana kwa ana katika barabara kuu ya Lagos-Ibadan.

Amesema makumi ya abiria wamejeruhiwa katika ajali hiyo na kwa sasa wanatibiwa katika Hospitali ya Adeoyo Yemetu mjini Ibadan.

Hii sio mara ya kwanza kwa ajali mbaya ya barabarani kufanyika katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Mwezi Mei mwaka huu, watu 26 walipoteza maisha katika ajali nyingine mbaya ya barabarani katika mji wa Lagos magharibi mwa Nigeria.

Basi lililogonga wanafunzi 11 na kuwaua papo hapo Nigeria Disemba mwaka 2016

Kwa mujibu wa takwimimu rasmi za Mamlaka ya Usalama Barabarani nchini Nigeria, zaidi ya watu elfu 5 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani nchini humo mwaka jana pekee.

Nchi ya Nigeria imekuwa ikikumbwa na visa vya ajali za barabarani kutokana na hali mbaya za magari, barabara pamoja na kutozingatiwa sheria za barabarani.