Israel ndiyo sababu kuu ya kujitenga Sudan Kusini
Balozi wa Sudan nchini Algeria amesema kuwa utawala ghasibu wa Israel ndiyo sababu kuu ya kujitenga Sudan Kusini na ardhi ya Sudan.
Isam Awadh Mutawalli amesema Sudan imekuwa ikikabiliwa na njama nyingi za nchi za Magharibi na utawala haramu wa Israel na kwamba kujitenga kwa Sudan Kusini ni miongoni mwa matokeo mabaya ya njama hizo.
Ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel na washirika wake walikuwa na njama ya kutaka kujitenga eneo la Darfur lililoko magharibi mwa Sudan na maeneo mengine kadhaa ya nchi hiyo lakini njama hizo zimegonga mwamba.
Kuhusu athari mbaya za kujitenga Sudan Kusini, balozi wa Sudan nchini Algeria amesema kuwa, Sudan ilipoteza asilimia 75 ya utajiri wake wa mafuta na uuzaji nje wa bidhaa hiyo umesimama.
Sudan Kusini ilijitenga na Sudan mwaka 2011 baada ya mapigano ya ndani yaliyoendelea kwa miongo kadhaa. Baada ya kujitenga na Sudan, nchi changa ya Sudan Kusini pia ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya Rais Salva Kiir wa nchi hiyo kumfuta kazi makamu wake wa zamani, Riek Machar kwa madai kuwa alifanya njama ya kumuondoa madarakani.