Watu 49 waghariki katika ajali ya boti mtoni kaskazini mwa Kongo DR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i44948-watu_49_waghariki_katika_ajali_ya_boti_mtoni_kaskazini_mwa_kongo_dr
Watu 49 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya boti kuzama mtoni kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 25, 2018 06:56 UTC
  • Watu 49 waghariki katika ajali ya boti mtoni kaskazini mwa Kongo DR

Watu 49 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya boti kuzama mtoni kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Richard Mboyo Iluka, Naibu Gavana wa Mkoa wa Tshuapa ameiambia Idhaa ya Radio Top Congo  kwamba, ajali hiyo ilitokea Jumatano, ambapo boti hiyo dhaifu ilizama ikiwa na makumi ya abiria.

Ameongeza kuwa, watu wengine 49 wamenusurika katika ajali hiyo iliyotokea jioni ya Jumatano iliyopita.

Boti iliyofurika watu kupindukia

Ajali za boti zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara DRC, na sababu kuu ya ajali hizo ni boti kujaza watu kupita kiasi na ubovu wa boti zenyewe. 

Aghalabu ya wananchi wa Kongo DR, nchi yenye misitu mingi inayoyahifadhi makundi ya waasi, hulazimika kutumia usafiri wa boti kwenye mito, katika safari za masafa marefu.