Uungaji mkono wa silaha wa Imarati kwa magaidi nchini Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47711-uungaji_mkono_wa_silaha_wa_imarati_kwa_magaidi_nchini_libya
Tovuti ya habari ya Tunisia Online Today imeripoti kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) inawapatia silaha magaidi huko Libya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 27, 2018 00:01 UTC
  • Uungaji mkono wa silaha wa Imarati kwa magaidi nchini Libya

Tovuti ya habari ya Tunisia Online Today imeripoti kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) inawapatia silaha magaidi huko Libya.

Tovuti hiyo ya habari ya Tunisia imewanukuu maafisa wa Libya na kuandika kuwa Imarati inawapatia fedha na silaha magaidi katika maeneo ya mpakani mwa Libya karibu na Tunisia katika mji wa Sabratha. Tovuti ya habari ya Tunisia Online Today imeongeza kuwa Imarati inafanya kila linalowezekana ili kuwapenyeza magaidi hao huko Algeria ili kuibua ukosefu wa amani nchini humo.  

Ghassan Salame Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Libya ametahadharisha mara kadhaa kuhusu uingiliaji kati wa nchi ajinabi huko Libya na kusisitiza kuwa uingiliaji kati huo unayakwamisha makundi ya Libya kufikia mapatano na kisha kusababisha hali ya mchafukoge nchini humo. Wakati huo huo tovuti ya Jane IHS iliwahi kuripori huko nyuma kuhusu hatua ya Imarati ya kuasisi kituo cha anga karibu na mji wa Marj mashariki mwa Libya; eneo ambalo linatumika kuruka ndege nyepesi za hujuma na zile zisizo na rubani.