Makumi ya magaidi wauawa na jeshi la Misri Peninsula ya Sinai
(last modified Fri, 17 May 2019 02:32:01 GMT )
May 17, 2019 02:32 UTC
  • Makumi ya magaidi wauawa na jeshi la Misri Peninsula ya Sinai

Jeshi la Misri limeangamiza magaidi 47 wenye mfungamano na kundi la kigaidi la Daesh katika operesheni ya vikosi vya usalama vya nchi hiyo katika mkoa wa Sinai Kaskazini.

Msemaji wa jeshi la Misri, Tamer al-Rifai amesema katika taarifa ya jana Alkhamisi kuwa, makumi ya magaidi wenye mfungamano na kundi la kigaidi la Daesh wameangamizwa katika eneo la Sinai Kaskazini la kufuatia operesheni ya siku kadhaa zilizopita iliyoendeshwa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo.

Taarifa hiyo ambayo haikuashiria ni lini hasa operesheni hiyo ilifanyika, imeeleza kwamba, wanajeshi 5 wa nchi hiyo wameuawa katika mapingano ya hivi karibuni.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, silaha kadhaa zimenaswa katika maficho ya magaidi hao, na mkwamba maafisa usalama wamefanikiwa kutegua mabomu yaliyokuwa yaliyokuwa katika maficho hayo.

Magaidi wa Daesh eneo la Sinai

Mapigano kati ya askari usalama wa Misri na watu wenye silaha katika mkoa huo wa Sinai Kaskazini ambayo yameua makumi ya raia na maafisa usalama yalishika kasi mwaka 2014 baada ya Rais Abdul Fattah al Sisi kushika madaraka ya nchi hiyo. 

Kundi la kigaidi linalojiita Wilaya ya Sinai ambalo ni tawi la kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh nchini Misri limekuwa likiendesha hujuma katika mkoa huo na limeshauwa makumi ya watu katika operesheni zake dhidi ya raia na askari wa kikosi cha ulinzi cha Misri. 

Tags