Hali ya hatari yatangazwa katika mpaka wa kusini mashariki mwa Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i53819-hali_ya_hatari_yatangazwa_katika_mpaka_wa_kusini_mashariki_mwa_tunisia
Serikali ya Tunisia imewaweka tayari askari jeshi wake wa ulinzi waliotumwa katika mipaka ya kusini mashariki mwa nchi hiyo na Libya.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
May 30, 2019 22:19 UTC
  • Hali ya hatari yatangazwa katika mpaka wa kusini mashariki mwa Tunisia

Serikali ya Tunisia imewaweka tayari askari jeshi wake wa ulinzi waliotumwa katika mipaka ya kusini mashariki mwa nchi hiyo na Libya.

Baadhi ya duru za kiitelijinsia zimetangaza kuwa Tunisia imepokea taarifa kutoka muungano wa kimataifa unaoendesha mapambano dhidi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh huko Iraq na Syria kwamba kiongozi wa kundi hilo Abubakar al Baghdadi yupo nchini Libya. Aidha duru za habari za Tunisia zimetangaza kuwa kiongozi huyo wa kundi la kigaidi la Daesh alikimbilia Libya kwa ajili ya hifadhi baada ya wapiganaji wake kupata kipigo kikali katika eneo la Baghur nchini Syria.  

Ripoti hiyo imeongeza kuwa wanajeshi wa uingereza walioko Libya pia wamepokea taarifa kuhusu kuwepo al Baghdadi nchini humo. Abubakar al Baghdadi mwishoni mwa mwezi Aprili uliopita alituma ujumbe kwa njia ya video katika vyombo vya habari vya Daesh; picha ambayo ilitajwa kuwa ya kwanza ya al Baghdadi kuonekana tangu mwaka 2014.