Uchaguzi wa bunge nchini Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i56457-uchaguzi_wa_bunge_nchini_tunisia
Mamillioni ya watu wa Tunisia leo wameshiriki katika uchaguzi wa bunge, ambao ni wa tatu tokea mapinduzi ya mwaka 2011 katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 06, 2019 12:12 UTC
  • Uchaguzi wa bunge nchini Tunisia

Mamillioni ya watu wa Tunisia leo wameshiriki katika uchaguzi wa bunge, ambao ni wa tatu tokea mapinduzi ya mwaka 2011 katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Upigaji kura ulianza mapema leo Jumapili asubuhi ambapo watu milioni saba wametimiza masharti ya kupiga kura.

Kuna wagombea 15,000 kutoka vyama vya kisiasa na wagombea huru ambao wanawania viti katika bunge la Tunisia lenye wajumbe 217.

Wapiga kura wanakusudia kuwachagua wanasiasa ambao wataboresha maisha na kuinua uchumi wa nchi hiyo.

Matokeo ya awali ya uchaguzi yanatazamiwa kutangazwa kuanzia Oktoba 10 huku matokeo rasmi yakitangazwa Novemba 17.

Baada ya hapo bunge hilo la Tunisia litakuwa na muhula wa miezi miwili kumchagua waziri mkuu mpya ambaye ataunda serikali.

Wagombea wawili wa uchaguzi wa Rais Tunisia Kais Saeid (kulia) na Nabil Karoui

Kwa mujibu wa sheria za Tunisia, chama kinahitaji kupata viti 109 ili kuunda serikali kwa kujitegemea, lakini uwezekano huo umetajwa kuwa mdogo katika uchaguzi  wa sasa.

Uchunguzi wa maoni umebaini kuwa bunge la Tunisia litatawaliwa na wagombea huru.

Uchaguzi wa leo Jumapili unafanyika wiki tatu baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais ambapo, wagombea wawili, Kais Saeid na Nabil Karoui, walipata kura za kutosha kuingia katika duru ya pili itakayofanyika Oktoba 13.