Rais wa zamani wa Kenya, Arap Moi ameaga dunia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i58934-rais_wa_zamani_wa_kenya_arap_moi_ameaga_dunia
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza mapema leo Jumanne kwamba, RAIS Mstaafu wa nchi hiyo, Daniel Toroitich Arap Moi, 1924 – 2020, amefariki dunia.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Feb 04, 2020 01:19 UTC

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza mapema leo Jumanne kwamba, RAIS Mstaafu wa nchi hiyo, Daniel Toroitich Arap Moi, 1924 – 2020, amefariki dunia.

Mzee Moi amefariki dunia katika Hospitali ya Nairobi ambako amekuwa akitibiwa mara kwa mara.

Rais Kenyatta ametangaza kuwa Mzee Moi, amefariki dunia leo asubuhi.

Msaidizi wa kibinafsi wa Mzee Moi, Lee Njiru pia amethibitisha kuwa Rais huyo wa pili wa Kenya ameaga dunia.

Rais Kenyatta anatarajiwa kutoa taarifa kamili baadaye kuhusu habari hiyo.

Moi alitawala Kenya kwa miaka 24 tangu 1978 hadi 2002.

Moi alikuwa rais wa Kenya kwa kipindi cha miaka 24 kabla ya kuacha madaraka mnamo 2002 baada ya Wakenya kumchagua kwa kura nyingi Mwai Kibaki aliyechukua nafasi ya Moi.

Daniel Arap Moi aliingia madarakani baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta.