Wafaransa walitumia mifupa ya wapigania uhuru wa Algeria kutengenezea sabuni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i64337-wafaransa_walitumia_mifupa_ya_wapigania_uhuru_wa_algeria_kutengenezea_sabuni
Mshauri wa masuala ya historia wa Rais wa Algeria amefichua jinai ambazo Ufaransa ilitenda nchini humo katika enzi za ukoloni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 31, 2020 00:30 UTC
  • Wafaransa walitumia mifupa ya wapigania uhuru wa Algeria kutengenezea sabuni

Mshauri wa masuala ya historia wa Rais wa Algeria amefichua jinai ambazo Ufaransa ilitenda nchini humo katika enzi za ukoloni.

Abdulmajid Shaykhi , mshauri wa Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria amefichua kuwa, wakati walipoikoloni nchi hiyo, Wafaransa walikuwa wakitumia mifupa ya wapigania ukombozi kutengenezea sabuni na kusafishia sukari.

Shaykhi ameongeza kuwa: baada ya kufanya mauaji, Wafaransa walikuwa wakiisafirisha mifupa ya Waalgeria waliouliwa nchini humo na kuipeleka mji wa Marseille huko Ufaransa.

Mshauri wa rais wa Algeria ameeleza pia kwamba, Wafaransa wanaizuia Algeria kuzirejesha nchini humo hifadhi za nyaraka na picha za enzi za ukoloni wa Ufaransa nchini humo.

Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria 

Rais wa Algeria amemwamuru Abdulmajid Shaykhi afanye mazungumzo na maafisa wa Ufaransa kuhusu mafaili ya zama wa ukoloni wa nchi hiyo huko Algeria kuanzia mwaka 1830 hadi 1962.

Kwa miaka minne sasa Ufaransa na Algeria zimo kwenye mazungumzo ya kujadili mafaili manne ya historia, lakini mazungumzo hayo hadi sasa hayajawa na tija yoyote; ambapo moja ya mafaili hayo linahusu hifadhi ya nyraka za Algeria ambazo maafisa wa seriali ya Ufaransa hawataki kuzikabidhi kwa nchi hiyo.../