Mahiga: Waliowashambulia Watanzania washitakiwa India
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i649-mahiga_waliowashambulia_watanzania_washitakiwa_india
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wa Tanzania, Dk. Augustine Mahiga ameliambia Bla nchi hiyo kuwa watu waliowashambulia Watanzania na kuwajeruhi vibaya nchini India wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 05, 2016 11:55 UTC
  • Mahiga: Waliowashambulia Watanzania washitakiwa India

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wa Tanzania, Dk. Augustine Mahiga ameliambia Bla nchi hiyo kuwa watu waliowashambulia Watanzania na kuwajeruhi vibaya nchini India wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

Waziri Mahiga amesema wanafunzi wanne raia wa Tanzania walioshambuliwa hapo jana huko India wametibiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitalini. Mwanadiplomasia huyo wa Tanzania amesema wizara yake imewasilisha malalamiko rasmi kwa serikali ya India kupitia balozi aliyeko Dar es Salaam na kwamba New Delhi imechukua hatua za haraka kuwakamata wahusika na kuwafikisha mahakamani.

Juzi Jumatano wanafunzi wanne raia wa Tanzania walishambuliwa na umati mkubwa wa watu nchini India baada ya Mhindi mmoja kupoteza maisha baada ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na raia mmoja wa Sudan. Kwenye tukio hilo, gari walilokuwa wakilitumia wanafunzi hao wa Tanzania lilichomwa moto huku msichana mmoja kati ya wanafunzi hao wanne akivuliwa nguo na kuburuzwa mtaani, jambo lililowakasirisha Watanzania wengi na raia wengine wa Afrika wanaoishi nchini India.