Rais wa Algeria asisitiza kuangamizwa utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i72384-rais_wa_algeria_asisitiza_kuangamizwa_utawala_wa_kizayuni
Rais wa Algeria jana usiku alifanya mazungumzo ya simu na Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na kusisitiza kuwa, nchi yake itaendelea kuwa bega kwa bega na Wapalestina hadi kuangamizwa maghasibu Wazayuni na kuundwa dola huru la Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 15, 2021 06:54 UTC
  • Rais Abdelmajid Tebboune
    Rais Abdelmajid Tebboune

Rais wa Algeria jana usiku alifanya mazungumzo ya simu na Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na kusisitiza kuwa, nchi yake itaendelea kuwa bega kwa bega na Wapalestina hadi kuangamizwa maghasibu Wazayuni na kuundwa dola huru la Palestina.

Rais Abdelmajid Tebboune ameitaja Palestina kuwa kibla cha kisiasa cha Algeria. Ramdane Lamamra Waziri Mpya wa Mambo ya Nje wa Algeria pia wiki iliyopita alisema kwamba: Taifa la Palestina linataka kuwa na amani na kwamba suala hilo linawezekana kwa kuasisiwa tu nchi huru ya Palestina yenye makao yake makuu katika mji mtukufu wa Quds.

Lamamra amesisitiza kuwa, ni wazi kuwa malengo matukufu ya wananchi wa Palestina ni sawa na nguzo ya mshikamamo kwa mataifa ya Kiarabu.  

Lamdane Lamamra, Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria 

Huko nyuma pia Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria ilitoa taarifa na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo kukabiliana na jinai dhidi ya binadamu zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina na matukufu yao.