Dec 07, 2022 15:17 UTC
  • Mwana wa rais wa zamani wa Msumbiji na maafisa 2 wa zamani wa intelijinsia wahukumiwa kifungo jela

Mahakama nchini Msumbiji leo imewakuhuku kifungo jela mwana wa kiume wa rais wa zamani wa nchi hiyo na wakuu wawili wa zamani wa intelijinsia kifungo cha miaka 12 kila mmoja kwa kuhusika na kashfa ya ufisadi ambapo serikali ilitaka kuficha madeni makubwa na kusababisha upoteaji wa fedha.

Gregorio Leao, mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama na Intelijinsia, Antonio do Rosario mkuu wa zamani wa kitengo cha upepelezi wa kiuchumi cha huduma ya usalama cha Msumbiji, na Ndambi Guebuza mwana wa kiume wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Armando Guebuza, ni miongoni mwa washtakiwa 19 katika kesi hiyo kubwa ya ufisadi kuwahi kuikumba Msumbiji. 

Ndambi Guebuza ahukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa ufisadi 

Washtakiwa 8 waliondolewa hatiani huku waliosalia walihukumiwa vifungo vya jela kuanzia miaka 10 hadi 12; katika shauri lililomchukua jaji muda wa wiki moja kulisoma. Akizungumza ndani ya chumba cha mahakama katika viwanja vya jela yenye ulinzi mkali katika mji mku wa Msumbiji, Maputo, Jaji Efigenio Baptista ameeleza kuwa, jinai zilizofanywa zimesababisha taathira ambazo madhara yake yataendelea kuviathiri vizazi vijavyo. 

Kashfa hiyo iliibuka baada ya kampuni zinazomilikiwa na serikali ya nchi hiyo maskini mwaka wa 2013 na 2014 kukopa kinyume cha sheria dola bilioni 2 (sawa na euro bilioni 1.9)  kutoka  benki za kimataifa ili kununua meli ya kuvua samaki aina ya tuna na meli nyingine za uchunguzi. Hata hivyo Serikali ililificha Bunge na wananchi mikopo hiyo ya mabilioni ya dola. 

Wakati deni lililofichwa lilipoibuliwa mnamo 2016, Shirika la Fedha Duniani  (IMF) na wafadhili wengine wa kimataifa walikata msaada wa fedha kwa Msumbiji na hivyo kuibua mgogoro katika deni kuu la taifa na kusababisha kuporomoka kwa sarafu ya nchi hiyo.

Tags