Makumi wauawa Nigeria katika mashambulizi ya Boko Haram
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i991-makumi_wauawa_nigeria_katika_mashambulizi_ya_boko_haram
Makumi ya watu wameuawa katika mashambulizi mawili ya bomu yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram huko kaskazini mwa Nigeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 11, 2016 00:08 UTC
  • Makumi wauawa Nigeria katika mashambulizi ya Boko Haram

Makumi ya watu wameuawa katika mashambulizi mawili ya bomu yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram huko kaskazini mwa Nigeria.

Maafisa wa usalama wa Nigeria wanasema kuwa, zaidi ya watu 60 wameuawa katika mashambulizi mawili ya mabumu yaliyolenga kambi ya wakimbizi kwenye mji wa Maiduguri ilioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Wamesema kuwa kambi hiyo inahifadhi wakimbizi waliolazimika kukimbia nyumba zao kutokana na mashambulizi ya Boko Haram.

Mashambulizi hayo yalitokea Jumanne iliyopita lakini habari zake zilichelewa kuripotiwa kutokana na kukatika kwa mawasiliano.

Ripoti zinasema zaidi ya watu 1650 wameuawa na kundi hilo la Boko Haram tangu Rais Muhammadu Buhari aapishwe kuwa rais wa nchi hiyo Mei 2015. Katika kampeni zake za uchaguzi, Buhari aliwaahidi Wanigeria kwamba ataliangamiza kundi hilo.

Kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram hivi karibuni lilitangaza tena mshikamano wake na kundi la kigaidi la Daesh linalofanya mauaji na ukatili wa kutisha katika nchi za Iraq na Syria.