Maelfu waandamana Washington kupinga ziara ya Netanyahu ; wataka kusitishwa mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza
(last modified Thu, 25 Jul 2024 03:17:24 GMT )
Jul 25, 2024 03:17 UTC
  • Maelfu waandamana Washington kupinga ziara ya Netanyahu ; wataka kusitishwa mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza

Maelfu ya watu wakiwemo Wayahudi wa Kimarekani jana waliandamana katika mji wa Washington wakati Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Israel alipokuwa akihutubua katika kikao cha pamoja cha Bunge la Kongresi ya Marekani.

Kabla ya Netanyahu kuhutubia Kongresi, waandamanaji walikuwa tayari wamefika makao makuu ya serikali ya Capitol Hill huku wakipiga nara " Palestina iwe huru, Palestina iwe huru huku wengine wakijaribu kuweka vzuizi barabarani. 

Askari polisi waliokuwa wamevalia barakoa za gesi waliuzuia kufika makao makuu ya serikali umati wa waandamanaji waliokuwa wakipiga nara wakitaka kusimamishwa vita na mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel huko Ukanda wa Gaza yaliyowauwa shahidi Wapalestina elfu 39 na kujeruhi wengine wengi hadi sasa. 

Maandamano dhidi ya ziara ya Netanyahu mjini Washington

Usiku wa kuamkia jana kikundi cha waandamanaji Wayahudi walifanya maandamano wakiwa wameketi mkabala wa jengo la ofisi ya Bunge la Kongresi. 

Waandamanaji mjini Washington  walikuwa wamebeba mabango yenye maandishi" mtendaji jinai Benjamin Netanyahu atiwe nguvuni". Wamesema Waziri Mkuu wa Israel anapaswa kutiwa mbaroni kama ilivyoagizwa na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai  mwezi Mei mwaka huu.

 

Tags