Mahudhurio ya kwanza rasmi ya Iran katika kikao cha Baraza la Kupambana na Ugaidi la Shanghai; hatua muhimu ya ushirikiano wa kiusalama nje ya mipaka
(last modified 2023-09-10T07:56:40+00:00 )
Sep 10, 2023 07:56 UTC
  • Mahudhurio ya kwanza rasmi ya Iran katika kikao cha Baraza la Kupambana na Ugaidi la Shanghai; hatua muhimu ya ushirikiano wa kiusalama nje ya mipaka

Kufuatia uanachama kamili wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, ujumbe kutoka Iran umeshiriki kwa mara ya kwanza katika mkutano wa 40 wa Baraza la Muundo wa Kieneo wa Kupambana na Ugaidi la jumuiya hiyo.

Tarehe 4 Julai, mkutano wa 23 wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai ulifanyika kwa njia ya mawasiliano ya Intaneti kwa uenyekiti wa India, na uanachama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika jumuiya hii ulitangazwa rasmi. Kwa msingi huo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikawa mwanachama wa tisa wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai.

Ingawa katika miaka ya hivi karibuni, hasa baada ya vikwazo vya Marekani kwa Russia na China, mwelekeo wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai katika ushirikiano wa kiuchumi umeongezeka, lakini jumuiya hii iliundwa kwa misingi ya usalama na ushirikiano wa kisiasa na katika umri wake wote ilifanya hima ya kufuata hili.

Haya ni mahudhurio ya kwanza ya Iran katika kikao cha Baraza la Muundo wa Kieneo wa Kupambana na Ugaidi wa jumuiya hii, ambacho kinafanyika miezi miwili baada ya Tehran kuwa mwanachama rasmi na radiamali nchi ya wanachama katika suala hili, ni kwamba, hii ni hatua muhimu katika ushirikiano wa usalama wa nje ya mipaka wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 

Kumechukuliwa misimamo ya maudhui mbili muhimu katika mkutano huu kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kwanza kabisa; nchi wanachama sambamba na kulaani mashambulizi ya kigaidi ya miezi michache iliyopita, likiwemo shambulio la Daesh dhidi ya Haram ya Shahcheragh washiriki wametoa mapendekezo ya kuzuia vitendo kama hivyo vya kigaidi.

Nukta ya pili ni kwamba, katika kikao hicho, kulitathminiwa na kushukuriwa juhudi za nchi za eneo katika kupambana na ugaidi na misimamo mikali na wahanga, vikosi na makamanda wa kijeshi akiwemo Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyeuawa shahidi na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran alitunukuliwa tuzo kutokana na mchango wake katika uwanja huo.

Kwa kutilia maanani kuwa kazi ya usalama ni kipaumbele kwa wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na pia kwa kuzingatia kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miongoni mwa wahanga wakubwa wa ugaidi duniani, Hapana shaka kuwa, uzoefu wa Tehran katika kupambana na ugaidi unaweza kusaidia katika kuimarisha utendaji wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai katika uga huo.

 

Kwa maneno mengine ni kuwa, Iran ikiwa na zaidi ya raia 17,000 waliouawa shahidi na makundi ya kigaidi likiwemo kundi la kigaidi la Mujahiden-e-Khalq, imegeuka kutoka kuwa mhanga na kuwa mpiganaji dhidi ya ugaidi. Kwa hivyo, kuwepo kwa Iran katika Jumuiya ya Shanghai, ambayo ni mahudhurio ya kwanza rasmi katika kikao cha baraza hilo la kupambana na ugaidi, kuna umuhimu mkubwa.

Kwa upande mmoja, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaweza kunufaika kwa kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo na kuhudhuria kikao cha Baraza la Muundo wa Kupambana na Ugaidi kwa ajili ya kufikia malengo yake ya kupambana na ugaidi, na kwa upande mwingine wanachama wa Shanghai wanaweza kunufaika na uzoefu wa thamani wa Iran katika uwanja huu.

Katika kikao kilichopita cha Jumuiya hii, ambacho kilifanyika kwa njia ya mawasiliano ya Intaneti kwa uwenyekiti wa, Waziri Mkuu wa Pakistan, Muhammad Shahbaz Sharif, akizungumzia maendeleo ya kikanda, alisisitiza jukumu muhimu la wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai katika kusaidia kuimarisha amani na utulivu na  mapambano ya pande zote dhidi ya ugaidi

Tags