Wito wa Iran kuelekea Siku ya Kimataifa ya Quds
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i10279-wito_wa_iran_kuelekea_siku_ya_kimataifa_ya_quds
Sambamba na kukaribia Siku ya Kimataifa ya Quds itakayoadhimishwa kote duniani kesho Ijumaa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa vikali jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 30, 2016 03:01 UTC
  • Wito wa Iran kuelekea Siku ya Kimataifa ya Quds

Sambamba na kukaribia Siku ya Kimataifa ya Quds itakayoadhimishwa kote duniani kesho Ijumaa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa vikali jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani hatua ya utawala ghasibu wa Israel ya kuendelea kukaliwa kwa mabavu ardhi za Wapalestina sanjari na kukivunjia heshima kibla cha kwanza cha Waislamu. Taarifa hiyo imesema: "Utawala wa Kizayuni unapanga njama ya kuyayahudisha kikamilfu matukufu ya Kiislamu na maneneo ya kihistoria ya Quds tukufu, ni jambo liisilokubalika namna askari wa utawala huo haramu wanavyovamia Masjidul Aqsa kila uchao mbele ya kimya cha jamii ya kimataifa." Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeongeza kuwa, ni wajibu wa kila Mwislamu kuunga mkono kadhia ya Palestina na kwamba, kuwaunga mkono Wapalestina na harakati za muqawama za Palestina katika barabara ya amani dhidi ya utawala wa Kizayuni, ni katika ajenda kuu ya maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu.

Hii ni katika hali ambayo, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya umuhimu wa Siku ya Kimataifa ya Quds na amewataka Waislamu hususan wananchi wa Iran kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya siku hiyo hapo kesho. Aidha Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu mbali na kutoa wito kwa wapenda haki duniani kujitokeza kwa wingi katika maandamano hayo imetangaza kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds inakumbusha njama za kimataifa dhidi ya Umma wa Kiislamu ambazo zilianza kwa kupandikizwa donda la saratani katika moyo wa Ulimwengu wa Kiislamu.