Kan'ani: Marekani imezitoa muhanga haki za binadamu kwa maslahi ya Israel
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: Marekani na nchi chache zimeuteka Umoja wa Mataifa na kutoa muhanga amani na usalama wa kimataifa kwa ajili ya maslahi ya utawala wa kibaguzi, ghasibu na unaotenda jinai wa Israel.
Nasser Kan'ani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema hayo katika radiamalii yake kwa mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya kambi ya Jabalia na kuweka picha za kambi hiyo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa "X" na kuandika: Kuharibiwa kwa kambi ya al-Bureij huko katikati ya Ukanda wa Gaza baada ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni, kunaonesha kina cha jinai na mauaji ya watu madhulumu wa Palestina.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: Idadi kubwa ya nchi, serikali na mataifa ya dunia yanataka kusitishwa mapigano na kukomeshwa mashambulizi mabaya na ya kiwendawazimu ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza. , isipokuwa serikali ya Marekani na serikali chache za Ulaya ambazo daima huingilia mambo ya ndani ya nchi zingine kwa nara ya kaulimbiu ya uwongo ya kutetea haki za binadamu.
Kanani Chafi amesema: Ni wazi kuwa Marekani na nchi chache zimeuteka Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na zimetoa muhanga amani na usalama wa kimataifa kwa ajili ya maslahi ya utawala wa kibaguzi na unaotenda jinai wa Israel.
Msemaji huyo wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesisitiza kuwa: Viongozi wa serikali ya Marekani na waungaji mkono wake wanawajibika sawa na maafisa wa utawala wa Kizayuni katika kutekeleza jinai zote hizo za kivita katika Ukanda wa Ghaza na ni lazima wawajibike.
Licha ya wito wa kimataifa wa kusitishwa vita mara moja katika Ukanda wa Ghaza, lakini utawala wa Kizayuni unaendelea na mashambulizi yake ya kiwendawazimu dhidi ya wananchi wa Palestina wanaodhulumiwa na wasio na ulinzi katika eneo hili.