Apr 05, 2024 07:52 UTC
  • Raisi: Tehran yaweka katika ajenda yake ya kazi ushirikiano na nchi zote za Kiislamu

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika dhifa ya (futari) Iftar na mabalozi wa nchi za Kiislamu wanaoishi Tehran kwamba suala la kushirikiana na nchi zote za Kiislamu lipo katika ajenda ya utendaji ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Shirika la habari la IRNA limeripotikuwa, Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana alasiri alikutana na kuzungumza na mabalozi na wafanyakazi wanaoziwakilisha nchi za Kiislamu hapa nchini katika kukaribia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds leo Ijumaa  na kusema: Kuimarisha uhusiano na majirani ni moja ya mihimili mikuu ya sera za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba sera za nje za Iran zinatoa kipaumbele katika suala la kuimarisha maingiliano ya kuboresha na kukuza maslahi ya pamoja na nchi za Kiislamu, na Tehran inatoa mkono wa kushirikiana na  majirani wote na nchi za Kiislamu. 

Rais wa Iran akizungumza na mabalozi na wafanyakazi wanaoziwakilisha nchi za Kiislamu hapa Iran 

Rais Raisi ameeleza kuwa moja ya changamoto za pamoja za nchi za Kiislamu na eneo hili ni uingiliaji wa nchi ajinabi kwamba nchi ajinabi zinatoa kipaumbele na kuzingatia sera, mitazamo na maslahi yao mkabala wa maslahi ya nchi za Kiislamu; na kamwe hazifikirii juu ya kuwaleteta furaha na kuzitatulia matatizo nchi za Kiislamu na watu wake.  

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa: Mababeru hawataki nchi za Kiislamu kushirikiana, kushikamana na kuwa na maelewano baina yao na hawapendi kuona nchi za Kiislamu zikikurubiana barabara.  

Tags