Jun 11, 2024 07:24 UTC
  • Tehran yalaani taarifa ya chuki dhidi ya Iran iliyotolewa na marais wa Marekani na Ufaransa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, amesema kuwa, yaliyomo katika taarifa ya chuki dhidi ya Iran iliyotolewa na marais wa Marekani na Ufaransa hayana msingi wowote bali yana malengo na misukumo ya kisiasa na ni mwendelezo wa siasa zilizoshindwa tangu zamani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Nasser Kan’ani Chafi, amelaani taarifa ya pamoja ya marais wa Marekani na Ufaransa, ambayo katika sehemu yake moja ina tuhuma zisizo na msingi na zisizokubalika dhidi  ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Iran yalaani taarifa ya chuki ya marais wa Marekani na Ufaransa dhidi ya Tehran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kuwa, nafasi inayojulikana sana ya Tehran katika kusimamisha na kuimarisha uthabiti na usalama katika eneo hili na duniani kiujumla pamoja na kupambana na magenge ya kigaidi kwa shabaha ya kuimarisha usalama wa kimataifa ni jambo lisiloweza kukanushika na kufafanua kuwa tangu ulipoanza mzozo wa Ukraine, sera ya wazi ya Iran daima imekuwa ni kusaidia utatuzi wa kisiasa wa tofauti zilizopo kati ya pande hizo mbili.

Amesema ni kichekesho kuona kwamba waungaji mkono wa utawala ghasibu wa Israel unaoua watoto kila siku na ambao umeshawauwa kwa umati na kuwachinja takriban watoto elfu 15,000 wa Kipalestina na maelfu ya wanawake katika kipindi cha miezi minane iliyopita, na ambao wanawakandamiza wanafunzi na wananchi wanaoandamana kupinga jinai za Israel, wanajipa uthubutu wa kuwafundisha wengine somo la maadili, sheria na haki za binadamu. 

Marais wa Marekani na Ufaransa wenye siasa za kindumilakuwili

Msemaji huyo wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amemshauri Rais wa Ufaransa arekebishe siasa za nchi yake dhidi ya Iran na aache kufuata kibubusa sera za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Tags