Rais wa Iran aelekea New York kushiriki katika mkutano wa UNGA
(last modified 2024-09-22T07:47:01+00:00 )
Sep 22, 2024 07:47 UTC
  • Rais wa Iran aelekea New York kushiriki katika mkutano wa UNGA

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameondoka Tehran na kuelekea New York, Marekani kwa lengo la kushiriki katika mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Rais Masoud Pezeshkian leo asubuhi ameondoka hapa Tehran na kuelekea New York Marekani akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa kisiasa wa nchi hii kwa lengo kushiriki katika Mkutano wa 79 wa UNGA. 

Rais Pezeshikian muda mfupi kabla ya kuelekea New York

Mbali na kushiriki na kuhutubia hadhara ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Pezeshkian pia atahudhuria kikao cha wakuu wa Mapatano Yajayo na pia atakuwa na mazungumzo na wakuu kadhaa wa nchi zinazoshiriki katika kikao cha 79 cha Baraza Kuu la UN. 

Rais wa Iran pia atakutana na makundi ya kisiasa, kijamii, kidini na vyombo vya habari na shakhsia wa Marekani ambapo ataweka wazi misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kujibu maswali yao. 

Tags