Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Iran amtunuku nishani ya Fat'h Kamanda wa Kikosi cha Anga cha IRGC
(last modified 2024-10-06T12:10:50+00:00 )
Oct 06, 2024 12:10 UTC
  • Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Iran amtunuku nishani ya Fat'h Kamanda wa Kikosi cha Anga cha IRGC

Ayatullah Ali Khamenei Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Iran amemtunuku nishani ya Fat'h, Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa Kikosi cha Anga na Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Nishani hiyo imetolewa kufuatia oparesheni iliyofanikiwa ya "Ahadi ya Kweli." 

Nishani ya Fat'h imeanzishwa kama nembo ya oparesheni za ushindi za wanamuqawama wa Kislamu na mashujuaa wa oparesheni hizo. Nishani hiyo imejumuisha ina majani matatu ya mitende na kuba la Msikiti Mkuu wa Khorramshahr na pia bendera ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.  

Nishati ya Fat'h

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, baada ya kujizuia kwa muda na kutochukua hatua kufuatia kukiukwa mamlaka ya kujitawala nchi hii na kuuliwa shahidi Ismail Haniyeh, Sayyid Hassan Nasrullah, Meja Jenerali Sayyid Abbas Nilfroushan aliyekuwa kamanda na mshauri wa ngazi ya juu wa IRGC huko Lebanon, na vilevile mauaji ya wanawake na watoto wasio na hatia huko Palestina na Lebanon; Jumanne iliyopita tarehe Mosi Oktoba, ilirusha mamia ya makombora ya balistiki katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) ikiwa ni jibu la kisheria na kwa mujibu Hati ya Umoja wa Mataifa.

Makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu yalilenga shabaha za kiusalama na kijasusi za utawala wa Kizayuni, na asilimia 90 ya makombora hayyo yalipiga maeneo yaliyokusudiwa kwa usahihi mkubwa. 

Tags