Jan 05, 2017 16:10 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Mashahidi Walinzi wa Haram ni fahari kwa taifa zima

Familia za makomandoo saba wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu la Iran waliouawa shahidi kwa ajili ya kulinda Haram ya Bibi Zainab (SA) iliyoko nchini Syria leo zilimtembelea Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Katika mkutano na familia za mashahidi hao saba, Ayatullah Khamenei amesema, mashahidi hao ni fahari na kitu cha kujivunia, si kwa jeshi pekee bali kwa taifa zima la Iran.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kuwa: "Katika kusindikiza maiti za waume zao, wake waheshimika wa baadhi ya mashahidi hao walitamka maneno ambayo yako juu ya kiwango cha ufahamu wa kawaida wetu sisi watu wa kimaada".

Wananchi wakisindikiza majeneza ya mashahidi watano Walinzi wa Haram

Ayatullah Khamenei ameashiria kuwa ni mashahidi hao Walinzi wa Haram ndio waliomsambaratisha adui na kufafanua kwa kusema: "Laiti kama waovu na wazushaji fitna, ambao ni vibaraka wanaotokana na uadui wa Marekani na Uzayuni, wasingekabiliwa na kuzuiliwa katika Haram ya Bibi Zainab (SA), tungelazimika kupambana nao Tehran, Fars, Khorasan na Esafahan.".../

Tags