Larijani: Iran na Russia kuendeleza ushirikiano wa kupambana na ugaidi
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mazunguumzo ya Tehran na Moscow kuhusu kupambana na ugaidi na ushirikiano wa pamoja katika uwanja huo utaendelea.
Dakta Ali Larijani alisema hayo jana Jumatatu alipokutana na kufanya mazungumzo mjini Moscow na Vyacheslav Volodin, Spika wa Bunge la Russia na kuwaambia waandishi wa habari kwamba, kuna ushirikiano wa pamoja kati ya Iran na Russia katika suala la kupambana na ugaidi na kwamba, nchi mbilzi hizo zimetoa pigo kubwa kwa magaidi hususan wa Daesh huko nchini Syria.
Spika wa Bunge la Iran amebainisha kwamba, Tehran imeshirikiana na Iraq katika vita dhidi ya ugaidi kwa takwa la nchi hiyo ya Kiarabu.
Dakta Ali Larijani amezungumzia matukiio ya Yemen na kusema kwamba, tangu awali Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikuwa ikisisitizia kupatiwa ufumbuzi kadhia ya nchi hiyo kwa njia za kisiasa, lakini baadhi ya madola yanataka kulipatia ufumbuzi tatizo hilo kupitia njia za kijeshi.
Kuhusiana na matamshi ya viongozi wa utawala ghasibu wa Israel ya kutaka kutoa pigo kwa maeneo ya Iran huko Syria, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema bayana kwamba, muamala wa utawala haramu wa Israel ni wa kkijeshi huko Syria na daima utawala huo umekuwa na muamala wa kivamizi mkabala na Syria.