Iran yazitaka Marekani na EU ziiondolee Syria vikwazo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61443-iran_yazitaka_marekani_na_eu_ziiondolee_syria_vikwazo
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametaka kuondolewa mara moja vikwazo haramu dhidi ya taifa la Syria vilivyowekwa na Marekani na Umoja wa Ulaya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 06, 2020 03:28 UTC
  • Iran yazitaka Marekani na EU ziiondolee Syria vikwazo

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametaka kuondolewa mara moja vikwazo haramu dhidi ya taifa la Syria vilivyowekwa na Marekani na Umoja wa Ulaya.

Sayyid Abbas Mousavi ametoa mwito huo jana Ijumaa na kusisitiza kuwa, hatua ya Marekani na Umoja wa Ulaya ya kurefusha vikwazo dhidi ya nchi hiyo ya Kirabu ni kinyume cha sheria na batili.

Mousavi amevitaja vikwazo hivyo kuwa jinai dhidi ya binadamu na ambavyo inaweka hatarini haki za binadamu za taifa la Syria.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria kuhusu uungaji mkono wa taifa la Iran kwa serikali na wananchi wa Syria na kubainisha kuwa, vikwazo hivyo sharti viondolewe ili wananchi wa Syria waweze kupata mahitaji yao ya msingi na waweze pia kuijenga upya nchi yao iliyoharibiwa na mashambulizi ya kigaidi.

Sehemu ya uharibifu wa hujuma za magaidi Syria kwa uungaji mkono wa US

Hivi karibuni, EU ilitangaza kurefusha vikwazo dhidi ya Syria hadi tarehe Mosi Juni mwaka 2021, kwa tuhuma kuwa eti serikali ya Damascus inakiuka haki za binaadamu. Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeashiria hatua ya Umoja wa Ulaya ya kurefusha vikwazo hivyo na kusema kuwa, ni kuifuata Marekani kwa njia ya kujidhalilisha na kwamba pia ni jinai dhidi ya binaadamu.

Hivi sasa watu 273 na taasisi 70 zenye uhusiano na serikali ya Syria zimewekwa katika orodha ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa tuhuma bandia. Tangu mwaka 2011 Umoja wa Ulaya na Marekani ikiwa ni katika fremu ya kuwaunga mkono magaidi, zimekuwa zikiiwekea Syria aina tofauti ya vikwazo.